Nenda kwenye maudhui
  • Ukurasa wa Mwanzo
    • Tuma ujumbe faraghaniEndelea kuwasilianaUnganishwa katika vikundiJielezeWhatsApp kwa ajili ya biashara
  • Faragha
  • Kituo cha Msaada
  • Blogu
  • Kwa ajili ya Biashara
  • Pakua
Pakua
Masharti na Sera ya Faragha2025 © WhatsApp LLC
Ukurasa Mkuu wa WhatsAppUkurasa Mkuu wa WhatsApp
    • Tuma ujumbe faraghani

      Ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho na vidhibiti vya faragha.

    • Endelea kuwasiliana

      Tuma ujumbe na upige simu bila malipo* kote ulimwenguni.

    • Unganishwa katika vikundi

      Utumaji ujumbe kwenye kikundi umerahisishwa.

    • Jieleze

      Jieleze kwa vibandiko, GIF, Picha na zaidi.

    • WhatsApp business

      Fikia wateja wako popote walipo.

  • Faragha
  • Kituo cha Msaada
  • Blogu
  • Kwa ajili ya Biashara
  • Programu
IngiaPakua
  • MUHTASARI
  • Mambo muhimu ya kuzingatia unapoanzisha jumuiya mpya au unapoongeza vikundi katika Jumuiya kwenye WhatsApp.

    • 100: Kuanzisha Jumuiya
    • 101: Kudumisha Usalama kwenye Jumuiya
    • 102: Jinsi ya Kusimamia Jumuiya Ipasavyo
    • 103: Jinsi ya Kukuza na Kushirikisha Jumuiya
  • Wawezeshe na kushirikiana na wasimamizi na wanajumuiya ili kujenga na kudumisha jumuiya inayowafaa.

    • 200: Kuweka Mipaka na Kudumisha Mazingira Bora ya Jumuiya
    • 201: Kudhibiti Migogoro na Kukuza Ushirikishwaji
    • 202: Kutekeleza Sheria za Jumuiya na Kuwadhibiti Wanachama Wagumu
    • 203: Kusimamia na Kugawa Majukumu kwa Jumuiya zenye wasimamizi wengi
  • Angalia jinsi watu kutoka sekta mbalimbali wanavyotumia WhatsApp kukuza jumuiya zao.

    • Wajenzi wa Jumuiya yetu
    • Jeshi la BTS Festapora
    • Mama wa Kiafrika nchini Deutschland
    • Lea Mtoto Mzuri
    • Jukwaa la Mtoaji
    • Soy Super Papa (Mimi ni Baba Bora)

Elimu

ITAKUCHUKUA DAKIKA 10 KUSOMA

Juma, mkuu wa shule ndogo, angependa kuwasiliana na walimu, wazazi na wanafunzi kwa urahisi na kwa njia inayohimiza utangamano. Amechoka kutuma barua pepe nyingi kwa vikundi tofauti na hafurahii kwamba mara nyingi watu hawazisomi. Huwa anawaona baadhi ya wazazi mara kwa mara, lakini ana wasiwasi kuhusu wale ambao huwa hawaoni. Je, wazazi hao wanafahamu fursa zote zinazopatikana kwa ajili ya watoto wao? Je, wao husoma kuhusu mikutano ya shule? Je, ni vigumu kwa wazazi hao kuwasiliana naye au timu yake?

Juma anakutana na walimu wenzake wanaofundisha vidato vya juu. Wanamweleza kuwa wazazi wengi huwasiliana nao moja kwa moja kuhusu shughuli za shuleni, na kwamba mara kwa mara wao hujadiliana na wazazi tofauti kuhusu masuala yale yale. Wakati huo huo, wanafunzi wengi wanahitaji kukumbushwa kila wakati kuhusu mitihani iliyoratibiwa, baadhi yao wameachwa nyuma kimasomo, nao wengine hawafiki shuleni. Walimu wanaunga mkono pendekezo la kuanzisha vikundi kwa kila kidato. Wanajiuliza iwapo kuna njia bora ya kuwasiliana na wazazi na wanafunzi, au hata kuanzisha vikundi vidogo vya kuwasaidia wanafunzi kimasomo na kuwawezesha kudumisha urafiki kati yao.

Baada ya kutathmini chaguo mbalimbali, Juma anaamua kutumia Jumuiya kwenye WhatsApp kwa kuwa itafaa zaidi. Itamsaidia kurahisisha mawasiliano kati ya walimu, wazazi na wanafunzi, na pia itakuwa njia nzuri ya kushirikisha na kuwasaidia wanafunzi wanaohitaji usaidizi. Kutumia WhatsApp ni rahisi na kila mtu atajiunga bila kutatizika.

  • Kabla hujaanzisha jumuiya, bainisha unalokusudia – je, ni kutoa taarifa kuhusu shughuli za shule, kutoa usaidizi kwa wanafunzi na walimu, kushiriki mbinu bora na nyenzo mpya za kufundishia, au kitu kingine? Lengo lako litakusaidia kubainisha wahusika utakaowajumuisha kwenye jumuiya na ni vikundi gani wataingia. Unaweza kuanzisha au kuongeza vikundi vifuatavyo:

    • vikundi vya walimu kulingana na kidato au somo;
    • kikundi cha wafanyakazi ambao si walimu;
    • vikundi vya wanaoshughulikia miradi tofauti;
    • vikundi vya wazazi kulingana na darasa au gredi;
    • vikundi vya wanafunzi kulingana na darasa, vikisimamiwa na walimu;
    • vikundi vya timu za michezo au shughuli nyingine za shule.

    Kuwa na lengo bayana la jumuiya kutawasaidia wasimamizi na wanajumuiya kuelewa sababu za kuongezwa au kutoongezwa kwa vikundi fulani. Kwa mfano, ikiwa lengo lako ni kushiriki taarifa kuhusiana na shule, unaweza kuongeza kikundi cha wazazi wa wachezaji wa timu ya soka ya shule, ili washiriki maelezo kuhusu vifaa vya michezo na ratiba za mazoezi. Kwa upande mwingine, kikundi cha wazazi ambao lengo lao ni kupiga soga kuhusu jambo linalowavutia hakitaongezwa.

    Huenda waliomo kwenye baadhi ya vikundi wakabadilika sana kila mwaka – kama vile vikundi vya darasa. Hili likifanyika, itakuwa rahisi kufunga kikundi na kuanzisha kingine kipya. Vikundi vingine, kama vile timu za michezo, vikundi vya masomo au miradi, huenda vikahitaji kuongezwa na kuondolewa mara kwa mara. Kuna uwezekano mkubwa wa kutobadilika kwa vikundi fulani kama vile muungano wa wazazi au wafanyakazi ambao si walimu, japo mara kwa mara wapo wanakikundi watakaoongezwa na wengine kuondolewa. Ikiwa vikundi vingi vinahitaji kuondolewa kila mwaka, huenda ikawa rahisi zaidi kufunga jumuiya na kuanzisha nyingine mpya.

  • Kudumisha mazingira mazuri ni muhimu kwa ustawi wa jumuiya yako. Iwe unazungumza na walimu, wazazi au wanafunzi, ni vyema kujumuisha Kanuni ya Maadili ya Jumuiya yako kwenye WhatsApp. Kanuni ya Maadili inajumuisha sheria, masharti, na maadili yanayoongoza jumuiya yako kufahamu tabia na maudhui yanayoruhusiwa na yasiyoruhusiwa kwenye jumuiya.

    Kwenye sekta ya elimu, yapo mambo fulani unayopaswa kutahadhari. Ni muhimu kuandaa mwongozo wa kina wa wasimamizi wa jumuiya na wa vikundi kuhusu:

    • Wanafunzi Wenye Umri Mdogo - Sharti mwanafunzi awe na umri wa angalau miaka 13 ili aruhusiwe kujisajili na kutumia WhatsApp, na katika Bara Ulaya, sharti awe amefikisha miaka 16. Jumuiya kwenye WhatsApp haipaswi kushirikisha wanafunzi walio chini ya umri unaoruhusiwa. Wasimamizi wanapaswa kufuatilia ikiwa kuna wanafunzi wenye umri mdogo, kisha waondoe akaunti za wanafunzi hao ikiwa zipo halafu waripoti kwa WhatsApp mara moja.
    • Viungo vya Mwaliko wa Kikundi na Wanakikundi Wapya - Viungo vya mwaliko vitakufaa sana kwa vikundi vya darasa na wazazi vinavyobadilika kila wakati. Hata hivyo, viungo vinapaswa tu kutumwa moja kwa moja kwa wanakikundi lengwa kupitia barua pepe au ujumbe wa faragha, pamoja na ilani ya kuonya dhidi ya kusambaza kwa wengine wasiohusika. Shirikiana na wasimamizi na wajumuiya kufuatilia na kumwondoa haraka yeyote asiyetambulika.
    • Uonevu - Uonevu unaweza kutokea kwa njia nyingi tofauti, kuanzia kueneza uvumi, kutuma picha zisizofaa, na kumtishia mtu. Chapisha matangazo mara kwa mara ili uwahimize wanajumuiya kuripoti uonevu kwa wasimamizi wa vikundi na wa jumuiya. Bainisha wazi kuwa uonevu hauruhusiwi kwenye jumuiya na utasababisha mwanajumuiya kuondolewa, na pia huenda ukapelekea mtu kuchukuliwa hatua kulingana na sera za shule dhidi ya uonevu.
    • Unyanyasaji wa Watoto - Pale ambapo watoto chini ya miaka 18 wanahusika, aina yoyote ya mawasiliano ya kingono ni kinyume cha sera za WhatsApp, na pia ni marufuku katika nchi nyingi. Hii pia inajumuisha watoto wachanga kushiriki picha zao za siri. Maudhui ya aina hii yanapaswa kufutwa mara moja. Wewe au wasimamizi mkipokea au mkiona maudhui yanayoonyesha mtoto akinyanyaswa au akidhulumiwa, wasiliana na kituo cha polisi cha eneo lako na Kituo cha Kitaifa cha Watoto Waliopotea na Wanaonyanyaswa (NCMEC), au Kituo cha Kimataifa cha Watoto Waliopotea na Wanaonyanyaswa (ICMEC), kisha uripoti na umzuie mtumiaji husika mara moja.

    Jinsi ya kuongeza na kuondoa watumiaji kwenye kikundi

  • Katika jumuiya za elimu, kunapaswa kuwepo na utaratibu maalum wa kuwateua wasimamizi wa jumuiya na wa vikundi, kuwasiliana na kuratibu shughuli miongoni mwa wasimamizi, na kuwajibika kwa wasimamizi wa vikundi katika kudhibiti vikundi vyao.

    Unapochagua msimamizi wa jumuiya, teua mtu ambaye kwa kiasi fulani ana uwajibikaji kwa jumuiya yako – kwa mfano, mwalimu au mfanyakazi aliyeajiriwa. Pia, angalia ujuzi na ufikiaji wa maelezo ambao msimamizi atahitaji ili kuhakikisha kuwa kuna mtiririko mzuri wa mawasiliano na kwamba yanayoshirikiwa ni muhimu kwa wanajumuiya.

    Kwa wasimamizi wa vikundi vya wazazi na wafanyakazi, unaweza kuteua msimamizi ambaye:

    • anazingatia Kanuni ya Maadili;
    • anatangamana na watu kwa urahisi, anapenda watu, na ni mstahimilivu;
    • yuko tayari kutenga muda wake kudhibiti kikundi;
    • yuko tayari kuwasiliana na kukutana na wasimamizi wengine mara kwa mara.

    Walimu wanapaswa kuteuliwa kuwa wasimamizi wa vikundi vya darasa vinavyohusisha wanafunzi walio chini ya miaka 18. Ikiwa kuna haja ya vikundi vidogo vya masomo au mradi, mwalimu anaweza:

    • kuhakikisha ndiye msimamizi wa kila kikundi;
    • kuchagua mwanafunzi mmoja awe msimamizi mwenza wa kikundi;
    • kuwasiliana na wasimamizi wenza wa vikundi vya wanafunzi mara kwa mara ili kujadili masuala yaliyopo na kuwakumbusha kuhusu Kanuni za Maadili;
    • kuwahimiza wanafunzi kumtaja kupitia alama ya @ katika soga au kumtumia ujumbe faraghani ikiwa wana malalamishi yoyote.
  • Ili kuwashirikisha wanajumuiya, ni muhimu kuhakikisha kwamba kinachoshirikiwa kwenye kikundi cha Matangazo ni muhimu na kinawahusu watu wote. Hii inaweza kujumuisha matangazo kuhusu:

    • mikutano au matukio;
    • likizo na kufunga shule;
    • uteuzi au mabadiliko kuhusu wafanyakazi;
    • mabadiliko ya mtalaa wa masomo;
    • tafiti za kupata maoni.

    Ni vyema kuzingatia madhumuni ya vikundi mbalimbali vilivyo kwenye jumuiya. Kutegemea malengo ya kikundi, unaweza kushirikiana na wasimamizi kutoa mwongozo kwa wanakikundi kuhusu watakachozungumzia, jinsi ya kuwasiliana, na mara ambazo wanapaswa kuchapisha maudhui. Huenda ikawa muhimu:

    • kutoa matangazo ya darasa kwa wazazi na wanafunzi kuhusu matukio, majaribio, na fursa zinazopatikana;
    • kutuma ujumbe kwa vikundi vya wazazi kulingana na darasa ili kuwaomba wajitolee, kuwaalika kukutana na walimu, au kujibu maswali wanayouliza mara kwa mara;
    • kutuma video za kuelimisha, hati za kazi ya kufanyia nyumbani, au kuwakumbusha kuhusu ratiba za mitihani kwenye vikundi vya darasa.

    Wasimamizi wa jumuiya na wa vikundi wanafaa kuwauliza wahusika maoni yao kuhusu maudhui wanayochukulia kuwa muhimu na yale ambayo wangependa kuona zaidi. Wasimamizi wa jumuiya na wa vikundi wanaweza pia kujadiliana katika kikundi cha Wasimamizi Pekee kuhusu mafanikio na changamoto, vikundi ambavyo wanafaa kuongeza au kuondoa ili mazungumzo yafanyike kwa ufanisi zaidi, na kubaini ikiwa matangazo fulani yanapaswa kushirikiwa katika kikundi au kwenye jumuiya.

Rudi kwa 203: Kudhibiti na Kupanga Majukumu kwa Jamii za Wasimamizi Wengi
Pakua mafunzo haya
Makala haya yamekusaidia?
NdiyoLa
Kwa nini makala haya hayakusaidia?
  • Makala haya yalikuwa na mkanganyiko
  • Makala hayatatui tatizo langu
  • Makala haya hainihusu mimi au jumuiya yangu
  • Makala hayaelezi jinsi ya kufanya hivyo kwenye WhatsApp
Asante kwa majibu yako.

INAYOFUATA

Vikundi vya Wanaotoa Usaidizi au Wanaojitolea
TAZAMA MAFUNZO
RUDI JUU
Pakua
Nembo Kuu ya WhatsApp
Nembo Kuu ya WhatsApp
Pakua
Huduma Zetu
VipengeleBloguUsalamaKwa Biashara
Sisi ni nani
Kutuhusu sisiKaziKituo cha ChapaFaragha
Tumia WhatsApp
AndroidiPhoneMac/PCWhatsApp Web
Unahitaji msaada?
Wasiliana NasiKituo cha MsaadaProgramuUshauri wa Usalama
Pakua

WhatsApp LLC 2025 ©

Sheria na Sera ya Faragha
Sitemap