Jinsi WhatsApp inavyoweza kukusaidia kukaa umeunganishwa wakati wa janga la virusi vya corona (COVID-19)
WhatsApp inakusaidia kujiunga na wale ambao ni muhimu zaidi kwako. Hapa kuna baadhi ya njia unazoweza kutumia WhatsApp kwa kuwajali marafiki na familia, pata habari rasmi za afya za hivi punde, na shiriki habari kwa uwajibikaji. Kama wewe ni mgeni kwa WhatsApp au unahitaji kozi ndogo, hapa kuna mwongozo wa hatua-kwa-hatua jinsi ya kuanza.
Viongozi wa Jumuiya
Tumejitolea kuwapa viongozi wa jamii msaada mkiwa mnapambana na changamoto hili. Jifunze unavyoweza kutumia WhatsApp kutaarifu na kuunganishwa na jumuiya yako wakati watu wana wasiwasi kuhusu virusi vya corona.
Hadithi
Tazama watu wanavyotumia WhatsApp kuwasiliana na jamii zao wakati huu wa changamoto:
Huko Pakistani, kikundi cha WhatsApp kilikusanya Rupia 21 milioni kusaidia jumuiya iliyokuwa inazama kwenye umasikini:
Soma makala hapa >Shule za msingi huko Naples, Italia zinaendelea na masomo licha ya kufungwa, kwa kutumia WhatsApp kuwasilisha kazi kwa familia:
Soma makala hapa >Huko Hong Kong mtu mmoja anatumia WhatsApp kushauri jamii kusaidia biashara za ndani:
Soma makala hapa >Programu ya kusaidia kupata kazi huko Yordani inatumia WhatsApp kushawishi wanawake kutafuta kazi wakati Virusi vya Corona vinashambulia:
Soma makala hapa >Wataalamu wa Afya huko Paris wameunda kikundi cha WhatsApp ili kupata habari za hivi punde kuhusu uwezo wa hospitali:
Soma makala hapa >Waalimu kwenye kambi za wakimbizi huko Siria wanashiriki masomo na wazazi kwa kutumia Whatsapp:
Soma makala hapa >Walioponea utumwa huko India wanatumia vikundi vya WhatsApp kuwaelemisha wenzao kuhusu virusi vya corona:
Soma makala hapa >Wagonjwa huko Florianópolis, Brazil wanaweza kufanya miadi na kuuliza maswali kwa kutumia WhatsApp:
Soma makala hapa >