Usalama wa WhatsApp

Faragha na Usalama vipo kwenye DNA yetu

Toka siku ya kwanza, tulitengeneza WhatsApp ili kukusaidia wewe uwe karibu na marafiki, kutoa taarifa muhimu wakati wa majanga asilia, kukuunganisha tena na familia ulizotengana nazo, au kutafuta maisha mazuri. Baadhi ya vipindi vya maisha yako binafsi umevishirikisha kwa WhatsApp, hii ndio sababu tumetengeneza fumbo la mwisho-kwa-mwisho kwenye matoleo ya karibuni ya programu yetu. Wakati fumbo la mwisho-kwa-mwisho linapotumika, jumbe zako, picha, video, jumbe za sauti, hati, na miito vinalindwa visiangukie kwenye mikono isiyo salama.

Usalama asilia

Fumbo la mwisho-kwa-mwisho la WhatsApp linafanya kazi wakati wewe na watu unaowatumia ujumbe mnapotumia matoleo ya mwisho ya programu yetu. Programu nyingi za kutumiana ujumbe zinafumba jumbe kati yako wewe na wao, lakini ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho wa WhatsApp unahakikisha wewe pekee na mtu unaye wasiliana naye ndio mtasoma kinachotumwa, na hakuna mwingine kati yenu, hata WhatsApp pia. Hii ni kwa sababu jumbe zenu zinalindwa kwa kufugwa, na ni mpokeaji tu na wewe ndio mna ufunguo maalum unao hitajika kufungua na kuzisoma. Kwa ulinzi wa ziada, kila ujumbe unaotuma una ufungaji na ufunguo wa pekee. Vyote hivi vinafanyika otomatiki: hakuna haja ya kuruhusu mipangilio wala kupangilia siri maalum kwenye soga ili kulinda jumbe zako.

Ongea kwa Uhuru

Miito ya WhatsApp inakuwezesha wewe kuongea na marafiki na familia yako, hata kama wapo nchi nyingine. Kama ilivyo jumbe zako, miito ya WhatsApp pia imefumbwa mwisho-kwa-mwisho kwa hiyo WhatsApp na upande wa tatu hawawezi kusikiliza.

Jumbe Zinazobaki na Wewe

Jumbe zako zinatakiwa kuwa kwenye mikono yako. Hiyo ndio sababu WhatsApp haihifadhi jumbe zako kwenye seva zetu wakati tumezipokea, na ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho unamaanisha WhatsApp na upande wa tatu hawawezi kuzisoma kwa njia yoyote.

Tazama Mwenyewe

WhatsApp inakufanya uangalie kama simu unazopiga na jumbe unazotuma zimefumbwa mwisho-kwa-mwisho. Kwa urahisi angalia kiashiria kwenye maelezo ya muwasiliani au maelezo ya kikundi.

Pata maelezo

Soma maelezo ya kina ya kiufundi ya ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho wa WhatsApp kwa ushirikiano wa Open Whisper Systems.