Toka siku ya kwanza, tumebuni WhatsApp ili kukusaidia kuwasiliana na marafiki, kushiriki taarifa muhimu wakati wa majanga ya asili, kuungana na wanafamilia mliopoteana, au kutafuta maisha mazuri. Baadhi ya matukio ya binafsi zaidi katika maisha yako hushirikishwa kwa kutumia WhatsApp, ndiyo maana tumebuni ufumbaji wa mwisho hadi mwisho kwenye programu yetu. Kwa kutumia ufumbaji wa mwisho hadi mwisho, ujumbe, picha, video, ujumbe wa sauti, nyaraka, na simu zako hulindwa ili zisiingie kwenye mikono isiyofaa.
Mfumo wa WhatsApp wa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho hutumika unapomtumia ujumbe mtu mwingine anayetumia WhatsApp Messenger. Ufumbaji wa mwisho hadi mwisho huhakikisha kuwa ni wewe na mtu unayewasiliana naye pekee ndio mnaoweza kusoma ujumbe au kusikiliza mawasiliano na kwamba hakuna mtu yeyote katikati, hata WhatsApp yenyewe. Hii ni kwa sababu kwa kutumia ufumbaji wa mwisho hadi mwisho, ujumbe wenu hulindwa kwa kufuli na ni wewe na mpokeaji pekee ndio mlio na ufunguo unaohitajika kufungua na kusoma ujumbe. Haya yote hufanyika kiotomatiki: hakuna haja ya kuwasha mipangilio au kupanga soga maalum za siri ili kudumisha usalama wa ujumbe wako.
Kila ujumbe wa WhatsApp hulindwa na itifaki ile ile ya ufumbaji wa Signal ambao hudumisha usalama wa ujumbe kabla haujatoka kwenye kifaa chako. Unapotuma ujumbe kwenda kwenye akaunti ya biashara ya WhatsApp, ujumbe wako huwasilishwa kwa usalama kwenda sehemu iliyochaguliwa na biashara hiyo.
WhatsApp inachukulia kwamba soga kati yako na biashara zinazotumia programu ya WhatsApp Business au zinazosimamia na kujihifadhia ujumbe wa wateja huwa zimefumbwa mwisho hadi mwisho. Mara tu ujumbe ukishapokelewa, utakuwa chini ya desturi za faragha za biashara husika. Biashara hiyo inaweza kuwapa idadi fulani ya wafanyakazi, au hata mashirika mengine, jukumu la kuchakata na kujibu ujumbe.
Baadhi ya biashara1 zitaweza kuchagua kampuni kuu ya WhatsApp, ambayo ni Facebook, ili ihifadhi kwa usalama na kujibu wateja. Unaweza kuwasiliana na biashara husika wakati wowote ili upate maelezo zaidi kuhusu desturi zake za faragha.
Malipo ya WhatsApp, ambayo yanapatikana kwenye nchi zilizochaguliwa, yanawezesha uhamishaji kati ya akaunti kwenye taasisi za kifedha. Kadi na namba za benki zinahifadhiwa zikiwa zimefumbwa kwenye mtandao wenye usalama sana. Hata hivyo, kwa kuwa taasisi za kifedha haziwezi kushughulikia miamala bila kupokea taarifa zinazohusiana na malipo haya, malipo haya hayakufumbwa kwa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho.
WhatsApp inataka kuhakikisha kuwa unaelewa kinachofanyika kwa ujumbe wako. Ikiwa hutaki kupokea ujumbe kutoka kwa mtu au biashara, unaweza kumzuia moja kwa moja kwenye soga au umfute kutoka kwenye orodha yako ya waasiliani. Tunataka kuhakikisha kuwa unaelewa jinsi ujumbe wako unavyoshughulikiwa na kwamba una hiari unazohitaji kufanya uamuzi unaokufaa.
Soma ufafanuzi wa kina wa kiufundi kuhusu ufumbaji wa mwisho hadi mwisho wa WhatsApp ulioundwa kwa ushirikiano na Open Whisper Systems.
Angalia Ushauri wa Usalama ili upate taarifa za mara kwa mara za usalama.
1 Mwaka wa 2021.