Kutoka siku ya kwanza, tumebuni WhatsApp ili ikusaidie uendelee kuwasiliana na marafiki, kushiriki maelezo muhimu wakati wa majanga ya asili, kuungana tena na wanafamilia mliotengana nao, au kutafuta maisha bora. Baadhi ya matukio ya binafsi zaidi katika maisha yako hushirikiwa kwa kutumia WhatsApp na ndiyo maana tumebuni ufumbaji wa mwisho hadi mwisho kwenye programu yetu. Kwa kutumia ufumbaji wa mwisho hadi mwisho, ujumbe, picha, video, ujumbe wa sauti, nyaraka, na simu zako hulindwa ili zisiingie kwenye mikono isiyofaa.
Mfumo wa WhatsApp wa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho hutumika unapomtumia ujumbe mtu mwingine anayetumia WhatsApp Messenger. Ufumbaji wa mwisho hadi mwisho huhakikisha kuwa ni wewe tu na mtu unayewasiliana naye mnaweza kusoma au kusikiliza ujumbe unaotumwa, na kwamba hakuna yeyote katikati, hata WhatsApp yenyewe. Hii ni kwa sababu kwa kutumia ufumbaji wa mwisho hadi mwisho, ujumbe wako hulindwa kwa kufuli, na ni wewe na mpokeaji pekee mlio na ufunguo maalum wa kuufungua na kuusoma ujumbe huo. Haya yote hufanyika kiotomatiki: hakuna haja ya kuwasha mipangilio au kupanga soga maalum za siri ili kudumisha usalama wa ujumbe wako.
Kila ujumbe wa WhatsApp hulindwa na itifaki ile ile ya ufumbaji wa Signal ambayo hudumisha usalama wa ujumbe kabla haujatoka kwenye kifaa chako. Unapotuma ujumbe kwenda kwenye akaunti ya WhatsApp ya biashara, ujumbe wako hufikishwa kwa usalama kwenye sehemu iliyochaguliwa na biashara hiyo.
WhatsApp inachukulia kwamba soga kati yako na biashara zinazotumia programu ya WhatsApp Business au zinazosimamia na kujihifadhia ujumbe wa wateja huwa zimefumbwa mwisho hadi mwisho. Mara tu ujumbe ukishapokelewa, utakuwa chini ya desturi za faragha za biashara husika. Biashara hiyo inaweza kuwapa idadi fulani ya wafanyakazi, au hata mashirika mengine, jukumu la kuchakata na kujibu ujumbe.
Baadhi ya biashara1 zitaweza kuchagua kampuni kuu ya WhatsApp, ambayo ni Meta, katika kuhifadhi ujumbe kwa usalama na kujibu wateja. Unaweza kuwasiliana na biashara husika wakati wowote ili upate maelezo zaidi kuhusu desturi zake za faragha.
Malipo ya WhatsApp, ambayo yanapatikana kwenye nchi zilizochaguliwa, yanawezesha uhamishaji kati ya akaunti kwenye taasisi za kifedha. Kadi na namba za benki zinahifadhiwa zikiwa zimefumbwa kwenye mtandao wenye usalama sana. Hata hivyo, kwa kuwa taasisi za kifedha haziwezi kushughulikia miamala bila kupokea taarifa zinazohusiana na malipo haya, malipo haya hayakufumbwa kwa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho.
WhatsApp inataka kuhakikisha kuwa unaelewa kinachofanyika kwa ujumbe wako. Ikiwa hutaki kupokea ujumbe kutoka kwa mtu au biashara, unaweza kumzuia moja kwa moja kwenye soga au umfute kutoka kwenye orodha ya unaowasiliana nao. Tunataka kuhakikisha kuwa unaelewa jinsi ujumbe wako unavyoshughulikiwa na kwamba una chaguo unazohitaji kufanya uamuzi unaokufaa.
Simu ya WhatsApp hukuwezesha kuzungumza kwa faragha na jamaa na marafiki, hata wakiwa katika nchi nyingine.
Ujumbe uliofumbwa mwisho hadi mwisho huhifadhiwa kwenye kifaa chako na wala si kwenye seva za WhatsApp baada ya kuwasilisha.
WhatsApp hukuruhusu uthibitishe kama simu unayopiga na ujumbe unaotuma umefumbwa mwisho hadi mwisho. Angalia tu kiashiria kwenye soga au katika maelezo ya unayewasiliana naye au maelezo ya biashara.
Soma maelezo ya kina ya kiufundi ya ufumbaji wa mwisho hadi mwisho wa WhatsApp, uliobuniwa kwa ushirikiano na Open Whisper Systems.
Angalia Ushauri wa Usalama kwa taarifa za mara kwa mara za usalama.
1 Mwaka wa 2021.