Faragha Yako ni Kipaumbele Kwetu. Tuma Ujumbe kwa Faragha.
Lengo letu ni kufanikisha mawasiliano duniani kwa njia binafsi kwa kubuni huduma ambayo ni rahisi na ya faragha. Iwe unatuma ujumbe wa binafsi kwa ndugu au marafiki, au unaandikia biashara, mawasiliano yako huwa salama kila wakati na ni wewe unayadhibiti.
Faragha kiotomatiki
Ufumbaji wa mwisho hadi mwisho
Mazungumzo yaliyo katika soga zilizofumbwa mwisho hadi mwisho huwa na rangi ya dhahabu; ujumbe na simu za aina hizi huwa kati yako na unayewasiliana naye, mtu mwingine hawezi kusoma wala kusikiliza, hata WhatsApp yenyewe haiwezi.
Ujumbe huhifadhiwa kwenye kifaa chako
Ujumbe wako ni wa kwako. Hiyo ndiyo sababu ujumbe wako unahifadhiwa kwenye simu yako, na hatuushiriki na watangazaji.
Unadhibiti faragha yako
WhatsApp inarahisisha kuelewa na kubadili faragha na usalama wako upendavyo.
Mwisho kuonwa
Chagua ikiwa unaowasiliana nao tu, kila mtu, au yeyote asione lini ulifungua WhatsApp mara ya mwisho.
Tumejitolea kudumisha usalama wako
WhatsApp inatoa mfuatano wa zana, vipengele, na rasilimali kukusaidia kufanya maamuzi sahihi na kuyaweka mawasiliano yako salama.
Pata maelezo kuhusu jinsi ya:
Kufanya vipengele vya usalama viwe unavyotaka kwenye Android | iPhone
Uwazi wa Data
Tunataka kueleweka vizuri kuhusu habari zinazobaki kuwa za faragha na habari tunazokusanya na kushiriki na kampuni yetu kuu, Meta. Taarifa tunazoshiriki hutusaidia kutoa hali bora ya utumiaji na kuboresha usalama. Kwa maelezo sahihi na ya hivi karibuni, angalia sera yetu ya faragha.