Lengo letu ni kuunganisha ulimwengu kibinafsi kwa kubuni bidhaa ambazo ni rahisi na binafsi. Iwe unatuma ujumbe wa binafsi kwa ndugu au marafiki, au unaandikia biashara, mawasiliano yako huwa salama kila wakati na ni wewe unayadhibiti.
Mazungumzo yaliyo katika soga zilizofumbwa mwisho hadi mwisho huwa na rangi ya dhahabu; ujumbe na simu za aina hizi huwa kati yako na unayewasiliana naye, mtu mwingine hawezi kusoma wala kusikiliza, hata WhatsApp yenyewe haiwezi.
Ujumbe wako ni wa kwako. Hiyo ndiyo sababu ujumbe wako unahifadhiwa kwenye simu yako, na hatuushirikishi kwa watangazaji.
WhatsApp inafanya kuwe rahisi kuelewa na kubadili faragha na usalama wako.
WhatsApp inatoa mfuatano wa zana, vipengele, na rasilimali kukusaidia kufanya maamuzi sahihi na kuyaweka mawasiliano yako salama.
Jifunze namna ya:
Tunataka kueleweka vizuri kuhusu habari zinazobaki kuwa za faragha na habari tunazokusanya na kushirikiana na kampuni yetu kuu, Facebook. Habari tunazoshirikisha zinatusaidia kutoa uzoefu bora wa mtumiaji na kuboresha usalama. Kwa taarifa zetu sahihi za hivi karibuni, angalia sera yetu ya faragha.