Pata usaidizi ukitumia Meta AI, iwe unapendelea maandishi au sauti—kuanzia kutatua tatizo la hisabati, hadi kuhariri picha au kutafuta mkahawa ambao kila mtu kwenye gumzo la kikundi anaweza kukubali.
Fanikisha mawazo yako kwa kutumia Meta AI kuhariri picha zako au kuunda picha mpya zinazoundwa na AI ili kutumia kama ikoni ya kikundi chako, kuweka kama mandharinyuma ya simu yako ya video, au kutuma kwenye gumzo.
Ujumbe ambao haujasomwa unapoanza kurundikana, Meta AI inaweza kusaidia kutoa muhtasari wao kwa haraka ili uweze kurudi moja kwa moja kwenye mazungumzo. Teknolojia ya Uchakataji wa Kibinafsi huwezesha Meta AI kuchakata ujumbe wako bila Meta au WhatsApp kuweza kuisoma.
Una udhibiti wa jinsi unavyotumia hali ya matumizi ya AI yanayopatikana kupitia WhatsApp. Kama kawaida, ujumbe na simu zako binafsi hulindwa na ufumbaji wa mwisho hadi mwisho. Kwa vipengele vinavyotumia ujumbe wako wa kibinafsi, teknolojia ya Uchakataji wa Kibinafsi huwezesha Meta AI kutoa jibu bila Meta au WhatsApp kuweza kusoma ujumbe wako.
Meta AI iko tayari kusaidia na kuna njia nyingi za kuitumia—iwe unauliza moja kwa moja ndani ya gumzo au kuchunguza matumizi mengine ya AI ndani ya WhatsApp.
Piga gumzo na Meta AI ili kujifunza, kuunda na kuchunguza. Kuanzia kufanya utafiti wa mahali utakapoenda katika likizo yako ijayo, hadi kuandika ujumbe kwa maneno yanayofaa, Meta AI inaweza kukusaidia.
Tumia Meta AI kuunda chochote unachoweza kufikiria, pakia selfi na ujiwazie katika hali yoyote na ushiriki matokeo na gumzo la kikundi chako.
Fanya picha zako zionekane jinsi tu ambavyo unataka zionekane. Ambia Meta AI iongeze mandharinyuma mapya, ondoa kipengele, kifanye kiwe kielelezo, na zaidi.
Iwe ulipiga picha ya mmea ambao hutambui au unahitaji usaidizi wa kuelewa dhana ya hisabati, tumia Meta AI ili kujifunza kuhusu kile kilicho kwenye picha zako.