WhatsApp ni njia ya haraka, rahisi na ya kuaminika ya kuwasiliana na mtu yeyote kote duniani. Zaidi ya watu bilioni 2 katika zaidi ya nchi 180 hutumia WhatsApp kuwasiliana na ndugu na marafiki, popote na wakati wowote. WhatsApp inatolewa bila malipo na inaweza kutumiwa kwenye vifaa mbalimbali katika maeneo ambako muunganisho ni dhaifu – hivyo inapatikana na inatumika popote ulipo. Ni njia rahisi na salama ya kushiriki matukio yanayokuvutia, kutuma taarifa muhimu au kuwasiliana na marafiki. WhatsApp huwawezesha watu kuwasiliana na kushiriki maudhui wakiwa popote duniani.
WhatsApp inajivunia Kutoa Fursa Sawa za Ajira kwa Watu Wote na Kuwajumuisha Wanaobauguliwa. Hatubagui kwa misingi ya kabila, dini, rangi, uraia, jinsia (ikiwemo ujauzito, uzazi, maamuzi kuhusu uzazi, au matatizo husika ya kiafya), mwelekeo wa ngono, utambulisho wa kijinsia, udhihirisho wa kijinsia, umri, hadhi ya mkongwe aliyelindwa, ulemavu, maelezo ya kijeni, msimamo au shughuli za kisiasa, au vigezo vingine husika vinavyotambulika kisheria. Ilani yetu ya Fursa Sawa za Ajira kwa Watu Wote inapatikana hapa. Pia, tunatoa nafasi za ajira kwa wanaowasilisha maombi ya kazi na wamehitimu licha ya kuwa wana historia ya uhalifu, kwa mujibu wa sheria husika ya kieneo, jimbo na kitaifa. Huenda tukatumia maelezo yako kudumisha usalama wa Facebook, wafanyakazi wake, na wahusika wengine kama inavyohitajika au kuruhusiwa kisheria. Unaweza kuangalia Sera ya Facebook kuhusu Maelezo ya Mapato na ilani kuhusu Sheria ya Fursa Sawa ya Ajira kwa Watu Wote kwa kubofya viungo husika. Pia, WhatsApp hushiriki kwenye mpango wa E-Verify katika maeneo fulani, kama inavyohitajika kisheria.
WhatsApp inajitahidi kutoa malazi yanayofaa kwa watuma-maombi wenye ulemavu katika mchakato wetu wa kuajiri. Ikiwa unahitaji usaidizi wowote au malazi kwa sababu ya ulemavu, tafadhali tujulishe kupitia accommodations-ext@fb.com .