Maandishi
Rahisi. Salama. Utumaji ujumbe wa kutegemeka.
Watumie ndugu na marafiki zako ujumbe bure*. WhatsApp hutumia muunganisho wa intaneti ya simu yako kutuma ujumbe kwa hiyo utaepuka matozo ya SMS.
Soga ya Kikundi
Vikundi hukuweka karibu
Kuwa karibu na vikundi vya watu walio muhimu kwako, kama vile familia au wafanyakazi wenzako. Kupitia soga za vikundi, unaweza kushiriki ujumbe, picha na video pamoja na hadi watu 256 kwa wakati mmoja. Pia unaweza kukipa jina kikundi chako, kutuliza au kuweka arifa maalum na zaidi.
WhatsApp Mtandaoni na kwenye Kompyuta ya Mezani
Fanya Mazungumzo Yaendelee
Kwa kutumia WhatsApp ya kwenye tovuti na kompyuta ya mezani, unaweza kusawazisha soga zako zote kwenye kompyuta yako kiulaini ili uweze kutuma na kupokea soga kwenye kifaa ambacho ni rahisi zaidi kwako. Pakua programu ya kwenye kompyuta au tembelea web.whatsapp.com uweze kuanza.
Simu za Sauti na Video za WhatsApp
Ongea kwa Uhuru
Kwa simu za sauti, utaweza kuongea na marafiki na familia bure*, hata kama wapo nchi nyingine. Kwa simu za video za bure*, utaweza kuwa na mazungumzo ya uso kwa uso wakati sauti au maandishi havitoshi. Simu za WhatsApp za sauti na video hutumia muunganisho wa intaneti ya simu yako, badala ya salio lako la muda wa maongezi, kwa hiyo huna haja ya kuhofia gharama za juu zinazohusishwa na upigaji simu.
Ufumbaji wa mwisho hadi mwisho
Usalama wa Asili
Baadhi ya matukio ya binafsi kabisa katika maisha yako hushirikiwa kupitia WhatsApp, hii ndiyo sababu tumetengeneza ufumbaji wa mwisho hadi mwisho kwenye matoleo ya karibuni ya programu yetu. Kwa kutumia ufumbaji wa mwisho hadi mwisho, ujumbe na simu unazopiga au kupokea huwa salama, kwa hiyo wewe tu na mtu unayewasiliana naye ndio mnaweza kusoma au kusikiliza. Hakuna mtu mwingine, hata WhatsApp yenyewe, anaweza kusoma wala kusikiliza.
Picha na Video
Shirikisha Nyakati zenye Umuhimu
Tuma picha na video kwenye WhatsApp papo hapo. Unaweza pia kunakili kumbukumbu muhimu kwako kwa kamera ya ndani. Kwa kutumia WhatsApp utatuma picha na video kwa haraka hata kama upo kwenye muunganisho wa polepole.
Ujumbe wa Sauti
Tamka Unachohisi
Wakati mwingine, sauti yako inaweza kuwasilisha ujumbe vizuri zaidi. Kwa mguso mmoja tu unaweza kurekodi Ujumbe wa Sauti, ni nzuri kwa salamu fupi au simulizi ndefu.
Hati
Ushirikishaji wa Hati Umefanywa kuwa Rahisi
Tuma PDF, hati, majedwali, maonyesho ya slaidi na zaidi, bila mahangaiko ya barua pepe au programu za kushirikisha faili. Unaweza kutuma hati za ukubwa wa hadi MB 100, kwa hiyo ni rahisi kufikisha unachotaka kwa unayemnuia.