Maandishi
Utumianaji Jumbe wa Kutegemewa, Rahisi
Tuma ujumbe kwa rafiki zako na familia bure*. WhatsApp inatumia muunganisho wa intaneti ya simu yako kutuma ujumbe kwa hiyo utaepuka tozo za SMS.
Soga ya kikundi
Vikundi kukuweka karibu
Kuwa karibu na vikundi vya watu wa muhimu zaidi, kama vile familia yako au wafanyakazi wenzako. Kwa soga za kikundi, unaweza kushirikisha jumbe, picha, na video hadi idadi ya watu 256 kwa wakati mmoja. Pia unaweza kukipa jina kikundi chako, kutuliza au kuweka arifa binafsi, na zaidi.
WhatsApp kwenye Tovuti na Desktopu
Fanya Mazungumzo Yaendelee
Kwa kutumia WhatsApp ya kwenye tovuti na desktopu, unaweza kuhamishia soga zako zote kwenye kompyuta yako kiulaini ili uweze kutuma na kupokea soga kwenye kifaa ambacho nirahisi zaidi kwako. Pakua programu ya desktopu au tembelea web.whatsapp.com uweze kuanza.
Simu za Sauti na Video za WhatsApp
Ongea kwa Uhuru
Kwa simu za sauti, utaweza kuongea na marafiki na familia bure*, hata kama wapo nchi nyingine. Na kwa simu za video za bure*, utaweza kuwa na mazungumzo ya uso kwa uso wakati sauti au maandishi havitoshi. Simu za WhatsApp za sauti na video zinatumia muunganisho wa intaneti ya simu yako, badala ya mpango wa dakika wa simu yako, kwa hiyo hauna haja ya kuwa na hofu kuhusu tozo zenye gharama za upigaji simu.
Ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho
Usalama kwa Asili
Baadhi ya vipindi vya maisha yako binafsi unayashirikisha kwa WhatsApp, hii ndio sababu tumetengeneza ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho kwenye matoleo ya karibuni ya programu yetu. Wakati umefumbwa mwisho-kwa-mwisho, jumbe zako na simu unazopiga au kupokea zipo kwenye usalama kwa hiyo wewe tu na mtu unayewasiliana naye ndiye atakayeweza kusoma au kuzisikiliza, na hakuna mwingine kati yenu, hata WhatsApp hawawezi.
Picha na Video
Shirikisha Nyakati zenye Umuhimu
Tuma picha na video kwenye WhatsApp papo hapo. Unaweza pia kuchukua nyakati muhimu kwako kwa kamera ya ndani. Kwa kutumia WhatsApp utatuma picha na video kwa haraka hata kama upo kwenye muunganisho wa polepole.
Jumbe za Sauti
Sema Kilicho Kwenye Akili Yako
Wakati mwingine, sauti yako inasema yote. Kwa mguso mmoja tu unaweza kurekodi Ujumbe wa Sauti, kamili kwa salamu ya haraka au hadithi ndefu.
Nyaraka
Ushirikishaji wa Hati Umefanywa kuwa Rahisi
Tuma PDF, hati, kurasajedwali, maonyesho-mtelezo na zaidi, bila mahangaiko ya barua pepe au programu za kushirikisha faili. Unaweza kutuma hati mpaka 100 MB, kwa hiyo ni rahisi kupata unachokihitaji kwa unayemtaka.