Watumie ndugu na marafiki ujumbe bila malipo*. WhatsApp hutumia muunganisho wa intaneti ya simu yako kutuma ujumbe, kwa hivyo utaepuka ada za SMS
.
Endelea kuwasiliana na vikundi vya watu walio muhimu sana kwako, kama vile familia au wafanyakazi wenza. Kwa kutumia soga ya vikundi, wewe pamoja na hadi watu 256 mnaweza kutumiana ujumbe, picha na video kwa wakati mmoja. Pia mnaweza kukipa kikundi chenu jina, kunyamazisha au kuweka mipangilio maalum ya arifa na mengine mengi.
Kwa kutumia WhatsApp kwenye wavuti na katika kompyuta, unaweza kusawazisha soga zako zote kwenye kompyuta yako kwa urahisi ili uendelee kuwasilina katika kifaa chochote kinachokufaa zaidi. Pakua programu ya kutumia kwenye kompyuta ya mezani au tembelea web.whatsapp.com ili uanze
Kwa kutumia simu za sauti, unaweza kuzungumza na ndugu na marafiki bila malipo* hata kama wako katika nchi nyingine. Isitoshe, simu za video bila malipo* zinakuwezesha kuwa na mazungumzo ya ana kwa ana wakati sauti au maandishi pekee hayatoshi. Simu za sauti na za video kupitia WhatsApp hutumia muunganisho wa intaneti ya simu yako badala ya kifurushi chako cha dakika za kupiga simu, hivyo kukuondolea hofu ya gharama kubwa za kupiga simu.
Baadhi ya mambo ya binafsi zaidi katika maisha yako hushirikiwa kwenye WhatsApp, ndiyo maana tumeunda ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho kwenye matoleo ya hivi karibuni ya programu yetu. Kwa kutumia ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho, ujumbe na simu zako hulindwa ili kuhakikisha kuwa ni wewe na mtu unayewasiliana naye pekee mnaoweza kusoma ujumbe au kusikiliza simu, na kwamba hakuna mtu yeyote katikati anayeweza kufanya hivyo, hata WhatsApp yenyewe.
Tuma picha na video kwenye WhatsApp papo hapo. Hata unaweza kupiga picha au kurekodi video ya nyakati muhimu kwako kwa kutumia kamera iliyo kwenye programu. Kwa kutumia WhatsApp, utatuma picha na video kwa haraka hata kama unatumia muunganisho usio na kasi ya juu.
Wakati mwingine, sauti yako ni mambo yote. Kwa mguso mmoja tu, unaweza kurekodi Ujumbe wa Sauti, njia mwafaka ya kutuma salamu za haraka au simulizi ndefu.
Tuma PDF, nyaraka, malahajedwali, maonyesho ya slaidi na mengine mengi bila mahangaiko ya barua pepe au programu za kushiriki faili. Unaweza kutuma nyaraka za ukubwa wa hadi MB 100, kwa hivyo ni rahisi kutuma unachotaka kwa unayemlenga.