Fanya mengi kwa pamoja ukiwa na Simu za WhatsApp
Unaposhiriki skrini, kuratibu simu na viungo, vya kupiga simu,
kuunganisha na kushirikiana katika muda halisi hakujawahi kuwa rahisi.
Endelea kufuatilia watu muhimu kwako kwa kupiga simu za video na za sauti bila malipo*, zinazotegemeka kote katika vifaa vya iOS na Android kimataifa.
* Unaweza kutozwa gharama ya data. Wasiliana na mtoa huduma wako ili kupata maelezo.
Unaposhiriki skrini, kuratibu simu na viungo, vya kupiga simu,
kuunganisha na kushirikiana katika muda halisi hakujawahi kuwa rahisi.
Ongea na marafiki na familia yako ukitumia simu ya sauti, au zungumza ana kwa ana ukitumia simu za video za ana kwa ana na za kikundi—hazina malipo * na hazina kikomo.
*unapopiga simu kwa kutumia WiFi au kifurushi cha data
Panga na muwe wabunifu pamoja kupitia skrini iliyoshirikiwa wakati wa simu za Video.
Unda Tukio ili uweke muda wa mkutano unaofaa kwa ratiba za kila mtu—ili mtu yeyote asikose.
Alika mtu yeyote kwenye WhatsApp ili ajiunge na simu yako kwa kumtumia kiungo cha kupiga simu.
Hangout za sauti za vikundi vya ukubwa wote. Iwe ni mchezo wa kandanda wa kusisimua, kukwama kwenye tatizo la kazi ya nyumbani au kushiriki habari kubwa, wakati mwingine unahitaji tu kuzungumza na yeyote anayepatikana kwenye soga yako ya kikundi.
Simu ya sauti hukuruhusu kuwapigia unaowasiliana nao simu bila malipo ukitumia WhatsApp, hata ikiwa upo nchi nyingine. Kupiga simu ya sauti kunatumia muunganisho wa intaneti wa simu yako badala ya dakika za mpango wako wa simu ya mkononi. Unaweza kutozwa ada za data. Ili kuanzisha simu, fungua gumzo la kikundi ambalo ungependa kulipigia na ubofye aikoni ya simu ili uanzishe simu yako. Unaweza pia kuchagua wasiliani walio nje ya gumzo zako za kikundi zilizopo kwenye Kichupo cha Kupigia Simu.
Kupiga simu ya video kunakuwezesha kuzungumza kwa video na watu unaowasiliana nao kutumia WhatsApp. Ili kuanzisha simu, fungua gumzo la kikundi ambalo ungependa kulipigia na ubofye aikoni ya simu video ili uanzishe simu yako. Unaweza pia kuchagua wasiliani walio nje ya gumzo zako za kikundi zilizopo kwenye Kichupo cha Kupigia Simu.
Kushiriki skrini huruhusu watu kushiriki kile kilicho kwenye skrini yao kwa wakati halisi. Ni lazima uwe kwenye simu ya video ili ushiriki skrini yako. Donoa Machaguo Zaidi (nukta tatu wima) katika vidhibiti vya video kisha uguse Shiriki skrini. Simu yako itaonyesha kidokezo kinachoonyesha kuwa unakaribia kuanza kurekodi ukitumia WhatsApp.
Unaweza kuunda matukio kwenye soga za binafsi au za kikundi ili kusaidia kupanga mikusanyiko na kuendelea kuwasiliana. Matukio yana maelezo muhimu ambayo yanaweza kupatikana kwa urahisi na watu. Ili kuunda tukio, Fungua gumzo yako binafsi au ya kikundi na ubofye Ongeza (ishara ya ongeza) > Tukio.
Vifaa vilivyounganishwa hutoa njia ya uhakika na salama ya kufikia WhatsApp kwenye kifaa chako chochote. Unaweza kuendelea kuunganishwa kwa kuunganisha hadi vifaa vinne kwa wakati mmoja kwenye simu yako kuu. Bado utahitaji simu yako kuu ili kusajili akaunti yako ya WhatsApp na kuunganisha vifaa vipya.