Nenda kwenye maudhui
  • Nyumbani
    • Tuma ujumbe faraghaniKaa mtandaoniJenga jumuiyaJielezeWhatsApp ya biashara
  • Faragha
  • Kituo cha Msaada
  • Blogu
Pakua
Masharti ya Huduma2023 © WhatsApp LLC
Ukurasa Mkuu wa WhatsAppUkurasa Mkuu wa WhatsApp
    • Tuma Ujumbe Faraghani

      Ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho na vidhibiti vya faragha.

    • Kaa mtandaoni

      Fikia wateja wako ulimwenguni.

    • Jenga jumuiya

      Mazungumzo ya kikundi yamerahisishwa.

    • Jieleze

      Jieleze kwa vibandiko, GIF, Picha na zaidi.

    • WhatsApp Business

      Fikia wateja wako popote walipo.

  • Faragha
  • Kituo cha Msaada
  • Blogu
WhatsApp WebPakua

Jinsi ya kuhamisha akaunti yako kutoka kwenye WhatsApp Messenger kuenda kwenye programu ya WhatsApp Business

Pakua na usanidi programu ya WhatsApp Business

1. Unda nakala ya akaunti yako ya WhatsApp Messenger: Ikiwa unahama kutoka akaunti ya WhatsApp Messenger kuenda kwenye WhatsApp Business, tunapendekeza uunde nakala. Kutounda nakala kunaweza kukakufanya upoteze soga zako zote. Fungua WhatsApp Messenger. Kwenye Android, gusa kisha uguse Mipangilio. Kwenye iPhone, gusa Mipangilio kwenye skrini yako ya soga. Kwenye Mipangilio, gusa Soga kisha Nakala za soga kisha Hifadhi nakala au Hifadhi nakala sasa. Ukisha maliza kuhifadhi nakala, nenda kwa hatua inayofuata.

2. Pakua na uzindue Programu ya WhatsApp Business: programu ya WhatsApp Business inaweza kupakuliwa bila malipo kwenye Duka la Google Play na Duka la Programu la Apple. Gusa ikoni ya WhatsApp Business kwenye skrini yako ya nyumbani.

3. Kagua Masharti ya Huduma: Soma Masharti ya Huduma ya WhatsApp Business, kisha gusa Kubali na Endelea ili kukubali masharti hayo.

4. Jisajili: WhatsApp Business hutambua kiotomatiki, nambari unayotumia kwenye WhatsApp Messenger. Ili kuendelea, gusa chaguo lililo na nambari yako ya biashara.

5. Hamisha akaunti yako: Acha programu yako ya WhatsApp Business wazi na simu yako ikiwa imewashwa mpaka mchakato wa kuhamisha akaunti ukamilike. Ingawa uhamisho hufanyika kiotomatiki, huenda ukaelekezwa kurejesha kutoka kwa nakala zako. Gusa Endelea au Rejesha. Kisha, gusa Inayofuata ikiwa utaelekezwa.

6. Toa ruhusa ya kuweza kufikia anwani na picha: Anwani zinaweza kuongezwa kwenye programu ya WhatsApp Business kutoka kwenye kitabu chako cha anwani. Pia, unaweza kutoa ruhusa ya kufikia picha, video na faili zilizo kwenye simu yako.

7. Unda akaunti: Jaza jina la biashara yako, chagua aina ya biashara, na uchague picha ya jalada.

8. Unda jalada lako la biashara: Gusa CHUNGUZA > Jalada la biashara. Hapa, unaweza kuongeza habari muhimu za biashara kama anwani yako ya biashara, maelezo, saa na mengineyo.

9. Anza kupiga gumzo. Sasa jalada la biashara yako limesanidiwa. Gusa au , kisha utafute au uchague mtu wa kutumia ujumbe. Andika ujumbe kwenye sehemu ya matini. Kisha, gusa au .

Gundua Zana za WhatsApp Business

Programu ya WhatsApp Business ina zana kadhaa za kukusaidia kuendesha biashara yako kwa ufanisi. Ili kugundua zana hizi, nenda kwenye skrini ya soga zako. Gusa Chaguo Zaidikwenye Android au Mipangilio kwenye iPhone. Kisha, gusa Zana za Biashara.

  • Katalogi: Tangaza na ushirikishe bidhaa na huduma zako kwenye akaunti yako ya biashara. Jifunze jinsi ya kuunda katalogi kwenye Android au iPhone.
  • Kiungo kifupi: Fanya iwe rahisi kwa wateja wapya kuwasiliana nawe. Watumie wateja wapya kiungo kifupi kilichoundwa kiotomatiki ili kuwawezesha kutumia biashara yako ujumbe. Jifunze jinsi ya kutumia viungo vifupi kwenye Android au iPhone.
  • Zana za kutuma ujumbe: Tumia violezo vya WhatsApp kuunda mapema mazungumzo ambayo ni muhimu sana. Unda ujumbe wa salamu otomatiki ili kuanzisha gumzo na wateja wapya. Weka ujumbe wa kuwa mbali ili kuwajulisha wateja wajue ni lini utarudi, au unda majibu ya haraka kujibu maswali yanayoulizwa mara kwa mara. Kwa taarifa zaidi kuhusu zana za kutuma ujumbe, soma makala yafuatayo:
    • Jinsi ya kutumia ujumbe wa salamu kwenye Android au iPhone
    • Jinsi ya kutumia ujumbe wa kuonyesha kuwa uko mbali kwenye Android au iPhone
    • Jinsi ya kutumia majibu ya haraka kwenye Android au iPhone
  • Lebo: Panga mawasiliano yako na wateja kwenye makundi yanayofaa, kama vile "Wateja wapya" au "Maagizo yanayosubiri kushughulikiwa." Jifunze jinsi ya kutumia lebo kwenye Android au iPhone.
Pakua
Nembo Kuu ya WhatsApp
Nembo Kuu ya WhatsAppPakua
Huduma ZetuVipengeleBloguHadithiKwa Biashara
Sisi ni naniKutuhusuKaziKituo cha ChapaFaragha
Tumia WhatsAppAndroidiPhoneMac/PCWhatsApp Mtandaoni
Unahitaji Msaada?Wasiliana NasiKituo cha MsaadaVirusi vya Korona
Pakua

WhatsApp LLC 2023 ©

Masharti ya Huduma