Ukurasa Mkuu wa WhatsAppUkurasa Mkuu wa WhatsApp
WHATSAPP WEB
VIPENGELE
PAKUA
USALAMA
KITUO CHA MSAADA

Chagua lugha yako

  • azərbaycan

  • Afrikaans

  • Bahasa Indonesia

  • Melayu

  • català

  • čeština

  • dansk

  • Deutsch

  • eesti

  • English

  • español

  • français

  • Gaeilge

  • hrvatski

  • italiano

  • Kiswahili

  • latviešu

  • lietuvių

  • magyar

  • Nederlands

  • norsk bokmål

  • o‘zbek

  • Filipino

  • polski

  • Português (Brasil)

  • Português (Portugal)

  • română

  • shqip

  • slovenčina

  • slovenščina

  • suomi

  • svenska

  • Tiếng Việt

  • Türkçe

  • Ελληνικά

  • български

  • қазақ тілі

  • македонски

  • русский

  • српски

  • українська

  • עברית

  • العربية

  • فارسی

  • اردو

  • বাংলা

  • हिन्दी

  • ગુજરાતી

  • ಕನ್ನಡ

  • मराठी

  • ਪੰਜਾਬੀ

  • தமிழ்

  • తెలుగు

  • മലയാളം

  • ไทย

  • 简体中文

  • 繁體中文(台灣)

  • 繁體中文(香港)

  • 日本語

  • 한국어

  • Pakua

  • Vipengele

  • Usalama

  • Kituo cha Msaada

  • Kuwa karibu

Jinsi ya kuanza kutumia WhatsApp Messenger

Pakua na usanikishe WhatsApp

1. Pakua na ufungue programu: Pakua WhatsApp Messenger bila kulipia kutoka kwenye Duka la Google Play au Duka la Programu la Apple. Ili ufungue programu, gusa aikoni ya WhatsApp katika skrini yako ya mwanzo.

2. Kagua Masharti ya Huduma: Soma Masharti ya Huduma na Sera ya Faragha, kisha gusa Kubali na Uendelee ili ukubali masharti.

3. Jisajili: Chagua nchi yako kwenye orodha kunjuzi ili uweke msimbo wa nchi yako, kisha weka nambari yako ya simu katika mfumo wa kimataifa wa nambari za simu. Gusa Nimemaliza au Inayofuata, kisha gusa Sawa ili upokee msimbo wa kujisajili wenye tarakimu 6 kupitia SMS au kwa kupigiwa simu. Kukamilisha usajili, weka msimbo wenye tarakimu 6. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kusajili nambari yako ya simu kwenye Android, iPhone au KaiOS.

4. Weka jalada lako: Kwenye jalada lako jipya, weka jina lako, kisha gusa Inayofuata. Unaweza pia kuweka picha ya jalada.

5. Ruhusu ufikiaji wa anwani na picha: Unaweza kuweka nambari za unaowasiliana nao kutoka kwenye kitabu cha anwani cha simu yako. Pia, unaweza kutoa ruhusa ya kufikia picha, video na faili zilizo kwenye simu yako.

6. Anzisha soga: Gusa au , kisha utafute mtu aliye kwenye anwani zako wa kuanza kupiga soga naye. Andika ujumbe kwenye sehemu ya matini. Ili utume picha na video, gusa au karibu na sehemu ya kuandikia ujumbe. Chagua Kamera ili upige picha au urekodi video mpya au Matunzio au Maktaba ya Picha na Video ili uchague picha au video iliyopo kutoka kwenye simu yako. Kisha, gusa au .

7. Unda kikundi: Unaweza kuunda kikundi chenye hadi washiriki 256. Gusa au , kisha Kikundi kipya. Tafuta au chagua washiriki wa kuwaongeza kwenye kikundi, kisha gusa Inayofuata. Charaza mada ya kikundi na uguse au Unda.

Njia mbalimbali unazoweza kuwasiliana

  • Ujumbe wa sauti: Ikiwa hutaki kuandika ujumbe, unaweza kutuma ujumbe wa sauti. Gusa na ushikilie au ili urekodi ujumbe. Kuacha kurekodi, achilia maikrofoni. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutuma na kucheza ujumbe wa sauti kwenye Android, iPhone au KaiOS.
  • Simu za sauti: Nenda kwenye kichupo cha Simu kisha uguse au . Tafuta unayetaka kumpigia simu. Gusa au ili uanze kupiga simu ya sauti. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kupiga simu ya sauti kwenye Android, au iPhone.
  • Simu za video: Fungua kichupo cha Simu kisha uguse au . Tafuta unayetaka kumpigia simu. Ili uanze kupiga simu ya video, gusa au . Pata maelezo kuhusu jinsi ya kupiga simu za video kwenye Android, au iPhone.

Vidokezo vya usalama na vipengele muhimu

Geuza sera na vipengele vya usalama vikufae
WhatsApp inafanya iwe rahisi kuelewa na kugeuza sera na usalama wako ili vikufae. Pata maelezo zaidi kwenye ukurasa wetu wa faragha.

Kagua ukweli wa habari unazopokea
Tafakari ikiwa ujumbe unaopokea ni wa kweli, kwa sababu huenda yote unayosikia yasiwe ni ya kweli. Ikiwa hujui mtu aliyetuma ujumbe ulioupokea, tunakuhimiza uyakinishe habari hizo kwa mashirika ya kukagua ukweli yanayoaminika. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuzuia usambazaji wa habari potofu kwenye makala haya.

Ujumbe uliosambazwa
Ili kusaidia kuzuia usambazaji wa habari potofu, tunaweka mipaka kwa jinsi unavyoweza kusambaza ujumbe. Unaweza kutambua ujumbe uliosambazwa kwa urahisi kwa kuwa una lebo ya Umesambazwa . Wakati ujumbe umesambazwa kutoka kwa mtumiaji mmoja hadi mwingine mara nyingi, ujumbe huo huashiriwa kwa aikoni ya vishale viwili . Unaweza kupata maelezo kuhusu mipaka ya kusambaza kwenye makala haya.

WHATSAPP

Vipengele

Usalama

Pakua

WhatsApp Web

Biashara

Faragha

KAMPUNI

Kuhusu

Kazi

Kituo cha Bidhaa

Kuwa karibu

Blog

Hadithi za WhatsApp

PAKUA

Mac/PC

Android

iPhone

MSAADA

Kituo cha Msaada

Twitter

Facebook

Virusi vya Korona

2022 © WhatsApp LLC

Faragha na Masharti