Ikiwa unafundisha shuleni au katika chuo kikuu, fikiria kujihusisha na wanafunzi wako kwenye WhatsApp ikiwa kusoma kumevurugwa.*
Tafadhali tumia WhatsApp kwa uwajibikaji unapowasiliana na wateja wako. Wasiliana tu na watumiaji unaowajua wanaotaka kupokea ujumbe kutoka kwako, waulize wateja wahifadhi namba yako ya simu kwenye kitabu chao cha anwani, na usitume ujumbe wa kiotomati au matangazo ya biashara kwa vikundi. Kwa kutofuata maadili bora ya kimsingi kunaweza kusababisha malalamiko kutoka kwa watumiaji wengine na uwezekano wa akaunti kupigwa marufuku.
Kama wewe ni mgeni kwa WhatsApp, bofya hapa kwa mwongozo wa hatua kwa hatua namna ya kuanza.
Kama una maswali yoyote kuhusu Kitovu cha Habari cha WhatsApp cha Virusi vya Corona, wasiliana nasi.