Vituo vya WhatsApp ni njia rahisi na ya faragha ya kupata taarifa muhimu kutoka kwa watu na mashirika unayoyajali.
Chunguza Orodha ya Vituo na ufuate vituo kuhusu mada zinazokuvutia, iwe ni za hivi punde kuhusu timu yako ya michezo uipendayo au bidhaa maalum kutoka kwenye duka la mkate katika eneo lako kila siku. Pata ufikiaji wa kipekee wa mambo unayopenda kwa kujisajili kwenye vituo unavyopenda*.
* Huenda kipengele kisipatikane kwa watumiaji wote.
Ni wewe tu unayeweza kuona vituo unavyofuata. Nambari yako ya simu itasalia ya faragha, na wasimamizi ambao umewahifadhi kama waasiliani pekee ndio wataweza kuiona.
Vituo vipo kwenye kichupo cha Masasisho, mbali na soga na simu zako za kibinafsi, na arifa za kituo zimenyamazishwa kwa chaguomsingi.
Shiriki masasisho na hadhira ya kimataifa yenye mabilioni ya watu na upate njia unayoweza kutegemea ya kujihusisha na kukuza wafuasi wako kwenye WhatsApp.
Tuma vibandiko maalum ambavyo hadhira yako inaweza kupakua, tuma ujumbe wa sauti ili kushiriki habari, au tumia kura za maoni kuwaalika wafuasi ili washiriki mawazo yao.
Shiriki kiungo cha kituo chako au msimbo wa kipekee wa QR kwenye Hali yako na katika soga zako za kibinafsi ili watu zaidi waweze kupata kituo chako.
Shiriki masasisho ya kipekee, ya wakati uo huo na wafuasi wako wanaohusika zaidi na wanaokuunga mkono sana huku ukichuma pesa, moja kwa moja kwenye WhatsApp.
* Huenda kipengele kisipatikane kwa watumiaji wote.