Unaweza kupakua programu ya WhatsApp Business bila malipo. Programu hii imeundwa kwa kuzingatia mahitaji ya wamiliki wa biashara ndogo. Programu hii inakurahisishia kuwasiliana na wateja wako moja kwa moja, kuangazia bidhaa na huduma zako na pia kujibu maswali ya wateja katika harakati zao za ununuzi. Andaa katalogi ili uonyeshe bidhaa pamoja na huduma zako na utumie zana maalum kuchuja na kujibu ujumbe haraka na kiotomatiki.
WhatsApp pia inaweza kuzisaidia biashara kubwa na za kati kutoa msaada kwa wateja na kuwasilisha arifa muhimu kwa wateja. Pata maelezo zaidi kuhusu API ya WhatsApp Business.
Unda jalada la biashara lenye maelezo yenye manufaa kwa wateja wako kama vile anwani yako, maelezo ya biashara, anwani ya barua pepe na tovuti.
Majibu ya haraka hukuruhusu kuhifadhi na kutumia tena ujumbe unaotuma mara kwa mara ili uweze kujibu maswali yanayoulizwa sana kwa haraka.
Panga anwani au soga zako zikiwa na lebo ili uweze kuzipata tena kwa urahisi.
Weka ujumbe wa kuashiria kwamba haupo wakati huwezi kujibu ili wateja wako wajue wakati wa kutarajia jibu. Unaweza pia kutunga ujumbe wa salamu ili kuitambulisha biashara kwa wateja wako.