
Programu ya WhatsApp Business
WhatsApp Business ni programu unayoweza kupakua bila kulipia, iliyoundwa kwa kuwazingatia wamiliki wa biashara ndogo. Programu hii inakurahisishia kutangamana na wateja wako moja kwa moja, kuangazia bidhaa na huduma zako, pamoja na kujibu maswali ya wateja katika mchakato wote wa ununuzi. Andaa katalogi ili uonyeshe bidhaa pamoja na huduma zako na utumie zana maalum kuchuja na kujibu ujumbe haraka kiotomatiki.
WhatsApp pia inaweza kuzisaidia biashara kubwa na za wastani kutoa usaidizi na kutuma arifa muhimu kwa wateja. Pata maelezo zaidi kuhusu API ya WhatsApp Business.