Kuhusu WhatsApp

Programu yetu

Zaidi ya watu bilioni 1 kwenye nchi zaidi ya 180 wanatumia WhatsApp1 kuwa karibu na marafiki na familia, wakati wowote na popote. WhatsApp ni bure2 na inakupa urahisi, usalama, utumaji jumbe na upigaji simu wa kutegemewa, inapatikana kwenye simu duniani kote.

1 Na ndio, jina WhatsApp ni la utani kutoka kwenye maneno What's Up.

2 Gharama za data zinaweza kutumika.

Dhamira yetu

WhatsApp ilianza kama mbadala wa SMS. Bidhaa yetu sasa inawezesha utumaji na upokeaji wa aina tofauti za media: maandishi, picha, video, hati, na mahali, pamoja na simu za sauti. Jumbe zetu na simu zinazopigwa zipo salama kwa ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho, inamaanisha kuwa hakuna upande mwingine wowote ukijumuisha WhatsApp unaoweza kusoma wala kuzisikiliza. Nyuma ya kila bidhaa maamuzi yetu ni kutaka watu waweze kuwasiliana sehemu yoyote duniani bila kuwa na mipaka.

Timu yetu

WhatsApp iligunduliwa na Jan Koum na Brian Acton ambao wakati wa nyuma walitumikia miaka 20 kwa pamoja pale Yahoo. WhatsApp ilijiunga na Facebook mnamo mwaka 2014, ila imeendelea kufanya kazi kama programu inayojitegemea yenye lengo la kuendelea kutengeneza huduma ya kutumiana ujumbe ambayo inafanya kazi kwa haraka na ya kutegemewa popote pale duniani.