Zaidi ya watu bilioni 2 katika zaidi ya nchi 180 wanatumia WhatsApp1 kuwa karibu na marafiki na familia wakati wowote na popote. WhatsApp ni bure2 na inakupa huduma ya kutuma ujumbe na kupiga simu kwa urahisi, usalama na kwa namna ya kutegemeka, inapatikana kwenye simu duniani kote.
1 Na ndio, jina WhatsApp ni la utani kutoka kwenye maneno What's Up.
2 Huenda ukatozwa ada za data.
WhatsApp ilianza kama mbadala wa SMS. Sasa huduma yetu inawezesha utumaji na upokeaji wa aina tofauti za midia: maandishi, picha, video, hati, na mahali, pamoja na simu za sauti. Baadhi ya matukio ya binafsi zaidi katika maisha yako hushirikishwa kupitia WhatsApp, ndiyo maana tumebuni ufumbaji wa mwisho hadi mwisho kwenye programu yetu. Kila uamuzi kuhusu bidhaa yetu huwa ni kwa lengo la kuwawezesha watu kote duniani kuwasiliana bila mipaka.
WhatsApp iligunduliwa na Jan Koum na Brian Acton ambao wakati wa nyuma walitumikia miaka 20 kwa pamoja pale Yahoo. WhatsApp ilijiunga na Facebook mnamo mwaka 2014, ila imeendelea kufanya kazi kama programu inayojitegemea yenye lengo la kuendelea kutengeneza huduma ya kutumiana ujumbe ambayo inafanya kazi kwa haraka na ya kutegemewa popote pale duniani.