Rahisi. Salama.
Utumaji jumbe wa kutegemewa.

Kwa WhatsApp, utapata uharaka, urahisi, utumaji jumbe na upigaji simu salama bure*, inapatikana kwenye simu dunia nzima.
Pakua sasa
* Gharama za data zitatumika. Wasiliana na mtoa huduma wako kwa maelezo.

Simu za Sauti na Video za WhatsApp

Ongea kwa Uhuru

Kwa simu za sauti, unaweza kuongea na marafiki na familia bure*, hata kama wapo kwenye nchi nyingine. Na kwa simu za video za bure*, unaweze kuwa na mazungumzo ya ana kwa ana endapo sauti au maandishi hazitoshelezi. Simu za WhatsApp za sauti na video zinatumia muunganisho wa intaneti ya simu yako, badala ya mpango wa dakika wa simu yako, kwa hiyo hauna haja ya kuwa na hofu kuhusu tozo zenye gharama za upigaji simu.

Ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho

Usalama wa Asili

Baadhi ya vipindi vya maisha yako binafsi umevishirikisha kwa WhatsApp, hii ndio sababu tumetengeneza fumbo la mwisho-kwa-mwisho kwenye matoleo ya karibuni ya programu yetu. Wakati mwisho-kwa-mwisho pamefumbwa, jumbe zako na simu unazopiga au kupokea zipo kwenye usalama kwa hiyo wewe tu na mtu unayewasiliana naye ndiye atakayeweza kusoma au kuzisikiliza, na hakuna mwingine kati yenu, hata WhatsApp hawawezi.
Chunguza vipengele